uundaji wa maneno - shahzade baujiti

Breaking

Monday, May 13, 2019

uundaji wa maneno

Kubainisha Mofimu katika Maneno
Bainisha mofimu katika maneno
Uambishaji ni nini?
Uambishaji wa maneno ni kitendo cha kupata maneno kwa kubandika Mofimu kwenye kiini cha neno. Uambishaji hutokea kabla ya kiini cha neno au mzizi wa neno. Mfano kiini pig- unaweza kuunda maneno kama inapiga, anayepiga, mpigaji, amepigika nk.
Mofimu zinazopachikwa katika mizizi huitwa Viambishi
Aina za uambishi
Kuna aina mbili za viambishi;
  1. Viambishi awali:Hivi ni viambishi vinavyo pachikwa kabla ya kiini/mzizi wa kitenzi.Kwa mfano anaimba, viambishi awali vya kitenzi anaimba -imba- ni a- na-
  2. Viambishi tamati:Hivi ni viambishi vinavyopachikwa baada ya kiini/mzizi wa kitenzi.Kwa mfano kitenzi anacheza, kiambishi tamati ni a- inayotokea baada ya z-
Dhima za Viambishi
  1. Viambishi awali:Hivi huonyesha nafsi, idadi na wakati.Mfano katika neno anaimbaa- inawakilisha nafsi, nafsi hiyo ni ya tatu.Vilevile, inaonyesha idadi, umoja, na inaonyesha wakati uliopo hali ya kuendelea.Vilevile , viambishi awali huonyesha uyakinishi au ukanushi .Kwa mfano , katika neno anaruka, a- huonyesha uyakinishi lakini katika hali ya ukanushi kitendo hicho kingebadilika na kuwa hataruka na kiambishi awali chake kingekuwa ha-.
  2. Viambishi tamati: Hivi hukamilisha maana ya neno. Kwa mfano kitenzi anakula kama kisingekuwa na kiambishi tamati -a, je neno anakul- lingeleta maana yoyote? Vilevile viambishi tamati huzalisha maneno mapya mfano wanacheza, wanachezeana.
MOFIMU
Fasili ya mofimu ni: Mofimu ni neno au sehemu ya neno yenye maana kisarufi, ambayo haiwezi kugawanyika zaidi bila kupoteza maana. Kwa mfano:
maneno
(a) babu, hewa
mofimu
kila neno lina Mofimu moja
AINA ZA MOFIMU
  1. Mofimu huru
  2. Mofimu tegemezi
MOFIMU HURU
Haya ni maneno kamili ambayo huwezi kugawa zaidi bila kupoteza maana.
Mfano:Baridi, kofia, hewa, kaka, mama, sana, maji. Maneno haya hayawezi kugawanyika zaidi na yakaendelea kuwa na maana hiyohiyo kisarufi.
MOFIMU TEGEMEZI
Ni vipande vidogovidogo vya maneno vyenye maana kisarufi. Mofimu hii maneno yamejengwa kwa kubandika vipashio kadhaa vya kisarufi ambavyo huweza kubadilishwa na maana ya neno ikabadilika.
Mfano: neno anapika lina mfano tegemezi ufuatazo
a
-na-
-pik-
-a
1
2
kiini
3
Mofimu zinazobadilika kwenye kiini cha neno huitwa Viambishi.
Katika lugha ya Kiswahili viambishi hutokea kabla na baada ya kiini cha neno.
Mfano
Wanapendana = Wa-na-pendan-a kiini cha neno ni-pend-.
Mofimu zilizobadilisha baada ya kiini –an-na-a viambishi vinavyotokea kabla ya kiini cha neno huitwa viambisha awali au tangulizi. Viambisha vinavyotokea baada ya kiini cha neno huitwa viambishi tamati au fuatishi.
Mfano
Bainisha mofimu katika maneno
Neno
Viambisha Awali
Kiini
Viambisha Tamati
Unapendelea
u-na-
-penda-
el-e-a
Waliongozana
wa-li-
-ongoz-
an-a
Analima
a-na-
-lim-
-a
anayeiimbisha
a-na-ye
-imb-
-ish-a

Dhima za Mofimu
Bainisha dhima za mofimu
Baadhi ya dhima za uambishaji ni kama ifuatavyo:
  1. Kuonyesha upatanisho wa usanifu maana ya maneno yanayozalishwa kutofautiana katika msingi wa kusanifu tu, lakini uhusiano wa maneno hayo hutokana na kiini au mzizi wake uleule.Mfano;Fundisha kiini chake ni fund. Unaweza kuzalisha maneno mengine kwa kutumia mzizi/kiini kilichopo kama vile fundishana, mafundisho, mfundishaji, fundishwa, fundishana.
  2. Uambishaji huonyesha nafsi
  3. Uambashaji huonyesha njeo (muda)
  4. Uambishaji huonyesha urejeshi
  5. Uambishaji huonyesha ukanushi
  6. Uambishaji huonyesha hali mbalimbali za kitenzi
Vitenzi vikiambishwa huweza kujenga/kuunda/kuzalisha vitenzi vingine au nomino.
Mfano
Bainisha dhima za mofimu
Vitenzi
Kiini
Nomino
Vitenzi
Cheza
-chez-
Mchezaji, mchezo
wanacheza/atamchezea
Piga
-pig-
Mpigaji, Mpiganaji
watanipiga, aliyempiga/wanaompiga
Uambishaji hutumika kuzalisha viwakilishi na vielezi.
Neno (Kiwakilishi)
Kiini
Kielezi
Huyu, Huyo
Hu
Humu, humo
Wangu, wako, wake
wa
Hii, hizo, hiki
hi
Viambishi awali vina dhima ya kudokeza nafsi, njia, idadi urejeshi na ukanushi.Mfano: Hawakulima
  • Ha-, kiambishi cha ukanushi
  • Ku-, kiambishi njeo/wakati
Viambishi tamati vina dhima mbalimbali hudokeza hali ya utendekaji, ukamilishaji au kimalizio cha neno na kauli za matendo kama vile kutendwa, kutendewa,kutendeka nk.
Dhima:Ukanusho, kutendeana, agizo na mtendwa, ukamilisho, usababishi.
Mfano
Bainisha dhima za mofimu
Neno
Viambishi Tamati
Anapiga
-a
Wanapigana
-an
Asipigwe
-w
Amempigisha
-ish-
Viambishi tamati vina dhima ya kutambulishwa mapema/nomino zilizoundwa kutokana na vitenzi.
Neno
Kiini
Viambishi Tamati
Piga
pig-
-o
Mchezo
chez-
-o
Mtembezi
tembe-
-z-i
Mfiwa
-fi-
-us-a

Kutumia Mnyumbuliko
Mazingira yanayosababisha Mahitaji ya Maneno Mapya
Elezea mazingira yanayosababisha mahitaji ya maneno mapya
Mnyumbulisho ni neno linalotokana na neno nyumbua. Kunyumbua kitu ni kuvuta, kuongeza urefu wa kitu hicho.
Kunyumbua katika lugha ya Kiswahili ni kuongeza vinyumbulishi katika katika kiini ili kupata msamiati mpya. Hivyo basi, mnyumbulisho ni njia mojawapo na inasaidia kuunda maneno kwa njia ya kunyumbulisha.
Viambishi vinapochukuliwa katika kiini cha neno, basi neno hilo huwa limenyumbulishwa. Kwa mfano neno lima kiini chake lim- huweza kunyumbulishwa na kupata maneno mengine mpya, kama lim-ishwa, lim-ia, lim-w-a.
Pia maneno ya mnyumbulisho yanaweza kuundwa kwa kuongeza viambishi kwenye shina, kwa mfano:
Neno
Kiini
Shina
Maneno ya Mnyumbuliko
Elekea
elek
eleka
Elekeana, elekea, elekwa, elekesha
Shikishana
shik
shikisha
Shikishana, shikisha, shikishaneni
Kwa ujumla tunawaza kusema kuwa maneno ya kawaida hunyumbulika. Hivyo kiini/mzizi au shina moja huweza kuzalisha maneno mengine mengi ambayo yanatokana na msingi mmoja wa maana.

Dhima ya Uambishaji na Mnyambulikoa wa Maneno
Fafanua dhima ya uambishaji na mnyambulikoa wa maneno
Dhima ya uambishaji ni kuleta upatanisho wa kisarufi, kuonesha idadi na umoja na wingi katika ngeli za majina, kuonesha njeo na kuonesha urejeshi pamoja na hali mbalimbali kwa uambikaji wa viambishi kabla ya mzizi wa neno. Aidha dhima ya mnyambuliko ni kuonesha matokeo ya tendo na kuzalisha kauli mbalimbali kwa kupachika viambishi baada ya mzizi wa neno.

Kuunda Maneno mbalimbali kwa kutumia Mnyambuliko
Unda maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambuliko
Uundaji wa maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambuliko hufanyika kwa kupachika viambishi baada ya mzizi wa neno na hivyo kulifanya neno husika liweze kuonesha matokeo mbalimbali ya matendo pamoja na kuzalisha kauli mbalimbali za matendo.
Activity
Unda maneno mbalimbali kwa kutumia mnyambuliko

Kutumia Maneno ya Mnyambuliko katika Miktadha mablimbali
Tumia maneno ya mnyambuliko katika miktadha mablimbali
Maneno ya mnyambuliko hutumika katika miktadha mbalimbali ambapo miktadha hiyo hujitokeza katika kauli mbalimbali za vitenzi. Kauli hizo ni kauli ya kutenda, kauli ya kutendwa, kauli ya kutendewa, kauli ya kutendea, kauli ya kutendeka, kauli ya kutendesha, kauli ya kutendana, na kauli ya kutendama.
Activity
Tumia maneno ya mnyambuliko katika miktadha mablimbaliLF

No comments:

Post a Comment